Jumapili 11 Mei 2025 - 19:19
Radi amali ya Hawza kutokana na Upuuzi wa Kubadili Jina la Ghuba ya Uajemi / Hawza ni Ngome Imara Dhidi ya Waharibifu wa Utambulisho wa Kitaifa wa Wairani

Hawza inapinga vikali aina yoyote ya uvamizi na upuuzi kuhusiana na kubadilisha jina la "Ghuba ya Daima ya Uajemi", na inasisitiza juu ya kutetea rasilimali za kitamaduni zilizopo eneo hili pamoja na hazina ya kidini na kitaifa za Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya taarifa kutoka Kituo cha Usimamizi wa Hawza ni kama ifuatavyo:

Wajibu muhimu wa hawza na maulamaa ni kusimama upande wa haki na kukabiliana na upotoshaji wa ukweli wa kihistoria na zaidi ya historia. Historia tukufu ya nchi yetu pendwa ya Iran imejaa jihadi na kujitolea kwa mashujaa wa ardhi hii katika kukabiliana na maadui ili kuondosha tamaa ya maadui hao. Hata hivyo, taifa hili shujaa limekuwa likikumbatia kwa moyo mpana mafundisho safi ya Uislamu, na daima limesimama pamoja na haki na ukweli.

Mfano dhahiri wa jambo hili ulijitokeza katika Vita vya Miaka Minane, ambapo watoto wa ardhi hii walijitolea kwa imani thabiti kwa ajili ya kulinda Iran ya Kiislamu, ili kulinda mali za nchi hii na utambulisho wake wa kidini na kitaifa. Ghuba ya Uajemi ni moja ya vielelezo vyenye thamani zaidi katika utambulisho wa kitaifa wa Iran pendwa na eneo hili, jina lake lina mizizi katika historia ya kale ya ardhi hii na limetajwa pia katika vitabu vya kihistoria.

Taifa kubwa na tukufu la Iran linaheshimu utamaduni, jiografia na rasilimali nyingine za mataifa mengine, na kamwe haliziangalii kwa jicho la tamaa. Hata hivyo, iwapo mtu yeyote atajaribu kunyoosha mkono wake kuelekea kwenye rasilimali za kimwili, kiroho au kihistoria za taifa la Iran, basi mkono wake utakatwa kama ilivyokuwa huko nyuma.

Kwa kila mmoja ni dhahiri kuwa hatua kama hizi ni muendelezo wa mtazamo wa kiharamia wa nchi za kikoloni wenye lengo la kueneza mfarakano kati ya mataifa, hususan mataifa ya Kiislamu. Ndugu zetu katika nchi za eneo hili wafahamu kuwa wakoloni si wenye uchungu na eneo hili, bali wanataka, kupitia mfarakano na migawanyiko miongoni mwa Umma wa Kiislamu, kuandaa mazingira ya kupora rasilimali tajiri zilizopo katika eneo hili na kulinda usalama wa utawala wa Kizayuni unaochukiwa, ili usidhoofike.

Umma wote wa Kiislamu na watu wote duniani ni mashahidi kuwa Irani imejitolea na kusimama kidete katika kuilinda Palestina na wanyonge duniani kote.

Hawza inapinga vikali aina yoyote ya uvamizi na upuuzi kuhusiana na kubadilisha jina la "Ghuba ya Daima ya Uajemi", na inasisitiza juu ya kuitetea rasilimali za kitamaduni zilizopo eneo hili pamoja na hazina ya kidini na kitaifa ya Iran.

Kituo cha Usimamizi wa Hawza

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha